Wakinga

Mwanamke na Mwanaume wa Kikinga

Wakinga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Njombe, Wilaya ya Makete.

Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni Wabena, Wakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.

Kabila la Wabena liko wilaya ya Njombe na eneo la Malangali likiwa linapakana na wilaya ya Ulanga na wilaya ya Kilombero (Mkoa wa Morogoro), Wakinga wako wilaya ya Makete na Wapangwa wako eneo la Malangali.

Yapo pia makabila madogo kama vile Wamahanji, Wakisi, Wamanda, Wamagoma n.k. ambao kwa ujumla wao wanachukua asilimia 6 iliyosalia ya watu Mkoani Njombe.

Lugha ya Wakinga inaitwa Kikinga. Asili ya lugha hii ina mkanganyo kidogo: baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa asili ya lugha hii ni misitu ya Kongo [1], huku taarifa nyingine zinaeleza kuwa asili ya jamii ya Wakinga ni Afrika Kusini na kwa waliingia Ukinga kwa kutokea mkoa wa Ruvuma.

Jamii ya Wakinga ina koo mbalimbali, kwanza ukoo wa Sanga, ambao ndio ukoo mkubwa na ndio uliokuwa unatawala jamii yote ya Wakinga. Koo nyingine ni pamoja na ukoo wa Kyando, Mahenge, Chaula, Tweve, Luvanda, Pila, Lwila, Ndelwa, Mlelwa, Mbilinyi, Msigwa na Mbwilo. Hizi ni baadhi tu ya koo za jamii ya Wakinga. [2]

  1. [1]
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-01-13. Iliwekwa mnamo 2024-01-13.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search